Siku ya Mtoto wa Afrika juni 16

SIKU YA MTOTO WA AFRIKA; TUSIMWACHE MTOTO NYUMA KATIKA KUPINGA UKATILI DHIDI YA WATOTO

Juni 16 kila mwaka bara la Afrika huadhimisha Siku ya Mtoto wa Afrika tangu kuidhinishwa kwa siku hiyo na Umoja wa Afrika mwaka 1991. Umoja wa Afrika ulianzisha Siku ya Mtoto wa Afrika kama sehemu ya kuwakumbuka na kutambua mchango wa watoto waliopoteza maisha katika mauaji yaliyotokea huko Soweto, Afrika ya Kusini wakati watoto walipoandamana kudai haki zao za msingi.

Kituo cha Kitaifa cha Utafiti na Machapisho ya Wanawake huungana na jamii ya kiafrika kuadhimisha siku hiyo maalumu katika kutambua mchango wa watoto katika jamii, sambamba na kuamsha uelewa wa serikali na jamii kwa ujumla katika kutetea haki za watoto ikiwemo haki ya elimu na haki nyinginezo.

Leave Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *